English Home Romanian Home
Electronic Bible Online Pages Multi Language Phone Application One Language d/">Download Ipod / MP4 Player Package Electronic Online Mobile Pages
Electronic Books Online Pages Build Ebook Phone Application Download Ebook Phone Application Download Desktop Application Download Ipod / MP4 Player Package Electronic Online Mobile Pages
Create Bible Application Create E-Books Application
Credits News
About our project   |    Mobile Pages   |   
Electronic Bibles / Swahili / Swahili Union Bible / Web / Hagai

Swahili

Printable ModePrintable Mode

Hagai, Chapter 1

1:1 Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake Hagai nabii, kusema,

1:2 Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana.

1:3 Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,

1:4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?

1:5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.

1:6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.

1:7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.

1:8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.

1:9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.

1:10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.

1:11 Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.

1:12 Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya Bwana, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama Bwana, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za Bwana.

1:13 Ndipo Hagai mjumbe wa Bwana, katika ujumbe wa Bwana, akawaambia watu, akisema, Mimi nipo pamoja nanyi, asema Bwana.

1:14 Bwana akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao;

1:15 katika siku ya ishirini na nne ya mwezi, katika mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa Dario mfalme.

Printable Mode

Seek to any passage:


Book:
Chapter:
Verse:


Search the text:


Search in:
Terms:
Case insensitive:

Multilingual Online Bibles

It is possible now to have the Holy Scriptures on your browser and to read it by using parallel display that will allow you to make comparisons between different translations or versions for a specific language. This occasion is unique, and you have only to add new parallel versions from the left side "Add parallel language" selector.


Select another version:


Add parallel versions:


Delete parallel versions:


Text source: This text is in the public domain, downloaded from http://www.unboundbible.org, compiled by biblephone2008@gmail.com.





free counters

Locations of visitors to this page






If you have any questions, remarks, suggestions, please contact me here. May God bless you in studying the Holy Scriptures.



Sitemap: Please select the BiblePhone modules in your language: